Tokyo. Ziara ilikuwa ya mafanikio asema Wen.
14 Aprili 2007Waziri mkuu wa China Wen Jiabao amekamilisha ziara yake ya siku tatu nchini Japan kwa kuzuru mji wa Kyoto.
Wen ametumia sehemu ya muda wake wa mwisho nchini Japan akicheza mchezo wa baseball katika chuo kikuu cha mji huo.
Baadaye alikula chakula cha jioni na kundi la wanasiasa wa mji huo pamoja na wafanyabiashara kabla ya kurejea mjini Beijing.
Kabla ya kuondoka , Wen amewaambia waandishi wa habari kuwa anaamini ziara yake, ambayo ilikuwa na lengo la kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili, imekuwa ya mafanikio.
Siku ya Alhamis , Wen alikuwa kiongozi wa kwanza wa China katika muda wa miongo miwili kuhutubia bunge la Japan. Ametoa ujumbe wa urafiki, huku akitoa onyo kwa Wajapan kutosahau mabavu yao waliyoonyesha wakati wa vita hali ambayo imeharibu uhusiano wao kwa muda mrefu.