Togo yadhihirisha dhamira ya kujiunga na Muungano wa AES
22 Machi 2025Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Togo Robert Dussey amekuwa akielezea wazi azma ya nchi yake kujiunga na Muungano wa Nchi za Sahel (AES) , akisisitiza kuwa uamuzi huo wa kimkakati unaweza kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kuwezesha ufikiaji wa bahari kwa mataifa ya Mali, Burkina Faso na Niger.
Muungano huo umekuwa katika mivutano na mataifa ya Ivory Coast na Benin, ukiyashtumu kwa kuwa karibu mno na nchi za Magharibi, na hivyo kulazimika kutumia bandari ya Togo.
Wataalam wa siasa za ukanda huo wanasema uanachama wa Togo katika muungano huo unaweza si tu kuwezesha ufikiaji wa bandari bali pia kufufua fursa mpya za biashara.