MigogoroAsia
Thailand na Cambodia zaendelea kushambuliana
27 Julai 2025Matangazo
Mataifa hayo yalitangaza nia hiyo ya kuumaliza mzozo baada ya Rais Marekani Donald Trump kujaribu kusuluhisha mzozo huo usiku wa kuamkia Jumapili.
Majirani hao wa Kusini-mashariki mwa Asia, ambayo ni mataifa yenye vivutio maarufu kwa mamilioni ya watalii wa kigeni, wameingia kwenye mzozo wao wa umwagaji damu kufuatia eneo la mpaka wa kaskazini mashariki linalozozaniwa.
Takriban watu 34 wamethibitishwa kuuawa huku wengine zaidi ya 200,000 wakilazimika kuyahama makazi yao. Shinikizo la kimataifa linaongezeka kuzitaka Cambodia na Thailand kufikia makubaliano ya kusitisha uhasama . Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezitaka pande zote kukubaliana mara moja kusitisha mapigano na kufanya mazungumzo ya kutafuta suluhu ya kudumu.