SiasaAsia
Thailand na Cambodia zaanza kujadili usitishaji mapigano
28 Julai 2025Matangazo
Video zimesambazwa katika mitandao ya kijamii zikimuonesha waziri mkuu wa Cambodia
Hun Manet na mwenzake wa Thailand Phumtham Wechayachai wakiwasili katika mji wa Malaysia wa Putrajaya.
Wakati huo huo, China leo imepongeza juhudi za kumaliza mapigano kati ya nchi hiyo mbili za Cambodia na Thailand.
Viongozi wa Thailand, Cambodia kukutana Malaysia
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo Guo Jiakun, amesema kuwa wanatumai kwamba pande zote mbili zitaanzia kwa kuangazia maslahi ya pamoja ya watu wao, kuthamini amani na ujirani mwema, kuwa watulivu na kusitisha mapigano haraka iwezekanavyo