Operesheni ya uokozi yaendelea Afghanistan baada ya tetemeko
1 Septemba 2025Hata hivyo juhudi hizo tayari zinakumbwa na changamoto kwa kuwa kuna baadhi ya maeneo yasiyofikika kwa urahisi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, limeliambia shirika la habari la AP.
Zaidi ya watu milioni 1.2 wameathirika na ama tetemeko kubwa au matetemeko hayo madogo, hii ikiwa ni kulingana na shirika la Marekani la masuala ya kisayansi la Geological Survey, lililorekodi karibu matetemeko madogo matano usiku mzima wa jana.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma salamu za pole, akisema anasimama pamoja na watu wa Afghanistan huku kongozi wa Kanisa Katoliki Papa Leo wa XIV akisema amesikitishwa sana na vifo vilivyotokana na tetemeko hilo
Tetemeko hilo la ukubwa wa kipimo cha 6.0 cha Richta limeathiri majengo kuanzia Kabul hadi mji mkuu wa Islamabad, nchi jirani ya Pakistan.