Tetemeko la ardhi lawaua watu 20 Myanmar na Thailand
28 Machi 2025Mjini Bangkok zaidi ya wafanyakazi 80 wamenasa kwenye kifusi cha jumba la ghorofa lililoporomoka kutokana na tetemeko hilo.
Akizungumzia athari za tetemeko hilo la ardhi, Marie Manrique ambaye ni mtaribu wa Shirikisho la Kimataifa la Mashirika ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) nchini Mynamar amesema.
"Tunajua, tunajua umeme na mawasiliano yamekatika katika maeneo kadhaa ya nchi. Shirika la Msalaba Mwekundu la Myanmar limeanzisha hatua za dharura, kwa hivyo tunao watu wanaojitolea kutoka kwenye shirika la Msalaba Mwekundu la hapa ; wako chini huko na kusaidia iwezekanavyo. kwa sasa wanahusika katika kile ninachoweza kusema ni tathmini za haraka sana na kujaribu kusaidia, iwezekanavyo. Hali ni ngumu sana lakini msaada wowote ambao wanaweza kutoa ni muhimu kwa wakati huu."
Mataifa mengine ya China, Cambodia, Bangladesh na India yameripoti tetemeko hilo ingawa hakuna taarifa za madhara makubwa. Muungano wa nchi za Ulaya tayari zimetangaza kujitolea kutoa msaada.