Tabia NchiAfghanistan
Zaidi ya watu 800 wafa kwa tetemeko nchini Afghanistan
1 Septemba 2025Matangazo
Kulingana na msemaji wa serikali ya Taliban, tetemeko hilo la ukubwa wa 6.0 katika kipimo cha richta limetokea Jumapili jioni na kuathiri miji kadhaa katika jimbo la Kunar, karibu na mji wa Jalalabad na kusababisha uharibifu mkubwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani Abdul Matin Qani ameliambia shirika la habari la AP kwamba pamoja na idadi hiyo ya waliokufa na kujeruhiwa kwenye eneo la Kunar, watu wengine wamekufa na mamia kujeruhiwa katika jimbo jirani la Nangarhar na nyumba nyingi zimeathirika.
Mkazi mmoja wa wilaya ya Nurgal iliyoathirika zaidi kwenye jimbo la Kunar amesema karibu kijiji chote kimeporomoka, na watoto na wazee wamefukiwa na vifusi.