JangaUrusi
Tetemeko kubwa la ardhi laipiga pwani ya mashariki mwa Urusi
30 Julai 2025Matangazo
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Jiolojia ya Urusi, tetemeko hilo ni kubwa kabisa kuwahi kulipiga eneo hilo la Rasi ya Kamchatka tangu mwaka 1952.
Tsunami iliyosababisha mawimbi makubwa ya bahari imeripotiwa katika visiwa vya Hokkaido vya Japan na visiwa vya Kuril vinavyomilikiwa na Urusi, na yanahofiwa kuelekea pia Ufilipino, Chile na Visiwa vya Solomon.
Tayari mataifa kadhaa katika pwani ya Bahari ya Pasifiki kama vile Ufilipino, Colombia na mengineyo yametangaza tahadhari ya kiwango cha juu ya kutokea Tsunami. Athari za tetemeko hilo zinatazamiwa kuonekana hadi nchini Marekani kwenye miji ya Carlifornia na Washington.