JangaAfghanistan
Tetemeko la ardhi Afghanistan: Waliokufa wapindukia 1,400
2 Septemba 2025Matangazo
Watu wengine zaidi ya 3,000 wamejeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi lililopiga katika miji kwenye jimbo la Kunar na mji wa Jalalabad.
Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 6.0 katika kipimo cha Richter lililopiga hapo jana, liliathiri pia majengo katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul na pia kwenye baadhi ya maeneo ya nchi jirani ya Pakistan.
Afisa wa Umoja wa Mataifa amesema vikosi vya uokoaji vinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na barabara zisizipitika na hivyo kuwa vigumu kuwafikia watu walioathiriwa. Afisa huyo amesema waokoaji wanajaribu kutumia helikopta lakini bado ni vigumu kuyafikia maeneo ya milima.