JangaAsia
Tetemeko jengine laupiga mji wa Mandalay, Myanmar
30 Machi 2025Matangazo
Watu katika maeneo ya mji wa Mandalay walisikika wakipiga mayowe wakati tetemeko hilo lililotokea. Siku ya Ijumaa tetemeko kubwa lililokuwa na ukubwa wa 7.7 ulipiga nchini Myanmar na kusababisha uharibifu mkubwa wa majengo na miundo mbinu.
Hadi sasa watu zaidi ya 1,600 wameuwawa na zaidi ya 3,400 hawajulikani waliko.
Tetemeko la ardhi lawaua watu 20 Myanmar na Thailand
Idadi ya walioangamia inatarajiwa kupanda kufuatia baadhi ya miili kuhofiwa kukwama chini ya vifusi vya majengo iliyoanguka. Waokoaji bado wanaendelea na shughuli ya kuwafuta manusura wa mkasa huo.