Tena mashambulio ya umwagaji damu nchini Iraq:
30 Novemba 2003Matangazo
BAGHDAD: Huko Iraq ya Magharibi wameuawa wanajeshi wawili wa Kimarekani na kujeruhiwa mwanajeshi mwengine uliposhambuliwa msafara wa magari yao ya kijeshi. Msemaji wa wanajeshi wa Kimarekani amearifu kuwa waasi waliushambulia kwa makombora ya mkono na mashinigani msafara huo uliokuwa karibu ya mpaka wa Syria, Mashariki mwa mji wa Husybah. - Kabla ya hapo walipigwa risasi na kuuawa maajenti saba wa Kispania, Kusini mwa mji mkuu Baghdad, msafara wao wa magari uliposhambuliwa kwa makombora ya mkono. Ajenti wa nane wa Kispania alisalimika baada ya kujeruhiwa. Na wanadiplomasia wawili wa Kijapani waliuawa iliposhambuliwa gari yao karibu ya mji wa Tikrit, ukiwa ni mji anakotoka mtawala aliyepinduliwa wa Iraq, Saddam Hussein. Serikali ya Ujerumani imelaumu vikali mashambulio hayo.