Ten Hag: Siwezi kuleta ufanisi Leverkusen kwa kiini macho
14 Agosti 2025Ten Hag ameyasema haya wakati ambapo anajiandaa kusimamia mechi yake ya kwanza kama kocha wa Leverkusen.
Kazi ya kwanza ya Ten Hag tangu kuachishwa kazi Manchester United inashuhudia muholanzi huyo kukabiliwa na kizingiti kikubwa cha kuijenga timu hiyo, kufuatia kuondoka kwa mtangulizi wake Xabi Alonso aliyeshinda taji la ligi.
Alonso aliondoka na wakafuatia wachezaji muhimu Jeremie Frimpong, Florian Wirtz, Jonathan Tah na Granit Xhaka.
"Najua jinsi ya kusimamia mchakato na siwezi kuulazimisha mchakato, haiwezekani. Hakuna mtu aliye kama Harry Potter," alisema Ten Hag Alhamis kuelekea mechi yake ya kwanza Ijumaa katika kombe la German Cup dhidi ya timu ya daraja la nne, Sonnenhof Grossaspach.
Alipokuwa United pia, Ten Hag alitumia kauli hiyo hiyo ya kutotumia kiini macho ili kupata ufanisi.