Tel Aviv. Makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika eneo la Gaza yafungwa kutokana na maandamano
30 Juni 2005Matangazo
.
Kumekuwa na mapigano zaidi katika mpaka wa Israel na Lebanon. Duru za kijeshi za Israel zimesema kuwa wanajeshi wa Israel wamehusika katika mapigano na wanamgambo wa Hizbollah wa Lebanon katika eneo la Shebaa . Hakuna ripoti za watu walioathirika , na msemaji wa Hizbollah amekana kuwa mapigano yanaendelea.
Ameviambia vyombo vya habari kuwa majeshi ya Israel yalifyatua risasi dhidi ya wapiganaji hao , lakini wao hawakurejesha mashambulizi. Hii inakuja siku moja baada ya Hizbollah kukishambulia kituo cha kijeshi cha Israel katika eneo hilo, na kumuua mwanajeshi mmoja.
Majeshi ya Israel yalirejesha mashambulizi hayo kwa mizinga na ndege za kivita.