TEL AVIV: Maandamano kudai uhuru wa mateka
1 Septemba 2006Matangazo
Maelfu ya waandamanaji mjini Tel Aviv wametoa mwito wa kuachiliwa huru wanajeshi 3 wa Kiisraeli waliotekwa nyara.Wamemtaka waziri mkuu wa Israel,Ehud Olmert aanzishe majadiliano kupata uhuru wa mateka hao na kuwarejesha kwa familia zao.Wanajeshi 2 walitekwa nyara na wanamgambo wa Ki-Lebanon wa Hezbollah kati kati ya mwezi Julai.Mwengine ametekwa nyara na wanamgambo wa Kipalestina tangu mwezi wa Juni.