TEHRAN:Umoja wa Ulaya yaeleza wasiwasi wake juu ya uamuzi wa Iran wa Nuklia
4 Agosti 2005Matangazo
Uingereza,Ufaransa na Ujerumani zimeiandikia serikali ya Iran barua zikielezea wasiwasi wao juu ya uamuzi wa kurejelea shughuli zake za kinuklia.
Mataifa hayo matatu yayouwakilisha Umoja wa Ulaya juu ya suala hilo yamesema Uamuzi wa Iran wa kuanzisha tena shughuli zake za Nuklia katika kiwanda chake kilichoko Isfahan huenda kukakiuka makubaliano yaliyoafikiwa mjini Paris pamoja na azimio lililoafikiwa na shirika la Nishati la kimataifa duniani.
Mataifa hayo pia yamesema kwamba Iran haina uwezo wa kutengeneza mafuta na kwa hivyo kufunguliwa upya kwa kiwanda chake huenda kukayafanya malengo yake muhimu ya mpango wa nuklia kutiliwa shaka.