TEHRAN:Uchaguzi wa Iran wazua hisia mbali mbali katika mataifa ya Magharibi
27 Juni 2005Matangazo
Kuchaguliwa kwa Ahmadnejad kuwa rais wa Iran kumezusha hisia mbali mbali miongoni mwa viongozi wa mataifa ya magharibi.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni amesema rais huyo mteule wa Iran sio mtu wa kupendelea Domokrasia wala uhuru.
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Yoschka Ficher pia ameelezea wasiwasi wake juu ya uchaguzi huo ulivyofanyika ikiwa ni pamoja na suala la kuzuliwa kusimama uchaguzini kwa wagombea kadhaa.
Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia masuala ya sheria na usalama Franco Frattini amesema chaguo la wairan Ahmadnejad ni pigo kubwa kwa wanamageuzi nchini humo.