TEHRAN.Kundi kuu la upinzani Iran lakanusha na mashambulio
13 Juni 2005Matangazo
Kundi kuu la Upinzani nchini Iran limekanusha kuhusika katika mashambulio mabaya ya Mabomu yaliyofanywa mjini Tehran na mji wa kusini magharibi wa Ahvaz,siku kadhaa kabla ya uchaguzi wa rais.
Katika shambulio hilo takriban watu wanane waliuwawa na zaidi ya wengine 70 walijeruhiwa.
Maafisa wa serikali walililaumu kundi hilo lililo mafichoni kwa kufanya mashambulio hayo
Ili kujaribu kuwafanya wapiga kura wasijitokeze kupiga kura.