Tehran. Vitisho vyaikasirisha Iran.
4 Septemba 2005Iran imekasirishwa na vitisho vya kimataifa vya kuiwekea nchi hiyo vikwazo kuhusiana na mpango wake wa kinuklia.
Serikali ya Iran imesema kuwa haitaacha kazi yake ya urutubishaji wa madini ya Uranium licha ya vitisho kuipeleka nchi hiyo katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa ajili ya kuadhibiwa.
Iran imerejea shughuli zake za kurutubisha madini hayo katika kinu chake kilichoko katika eneo la Isfahan mwezi uliopita baada ya kukataa vivutio vilivyotolewa na mataifa ya umoja wa Ulaya.
Ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na shirika la kimataifa la nishati ya Atomic imesema kuwa Iran imetengeneza karibu tani saba za gesi inayohitajika kurutubisha Uranium.
Marekani , ambayo inaishutumu Iran kwa kutana kwa siri kutengeneza silaha za kinuklia , inataka nchi hiyo kufikishwa katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.