Tehran. Uchaguzi wa ziara utafanyika tena Iran hapo Ijumaa baada ya wagombea saba kutopata wingi wa kutosha.
19 Juni 2005Waziri wa mambo ya ndani wa Iran ametangaza kuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Akbar Hashemi Rafsanjani na kiongozi mwenye msimamo mkali Mahmoud Ahmadinejad watapambana katika uchaguzi wa ziada kwa ajili ya kiti cha urais nchini humo.
Matokeo rasmi yanampa Bwana Rafsanjani , ambaye anaonekana kuwa ni mwenye msimamo wa wastani, asilimia 21 ya kura katika duru ya kwanza.
Aliweza kumpita kwa asilimia ndogo mpinzani wake mkuu, meya wa Tehran na muungaji mkono mkuu wa uongozi wa kidini wa Iran . Watu waliojitokeza katika uchaguzi uliofanyika siku ya Ijumaa walikuwa asilimia 62 idadi ambayo ni chini kuliko ilivyotarajiwa.
Msemaji wa baraza la utawala , ambalo ndilo linaandaa uchaguzi amesema kuwa uchaguzi huo wa duru ya pili utafanyika siku ya Ijumaa.