TEHRAN: siwezi kuachana na mpango wa Nuklear asema rais wa Iran
31 Machi 2005Matangazo
Rais Mohammad Khatami wa Iran amewatembeza wandishi habari katika maeneo ya nuklea yanayolindwa kwa karibu.
Rais Khatami ameapa kwamba nchi yake haitasimamisha mpango wake wa silaha za kinuclea. Amewaambia wandishi habari kwamba licha ya shinikizo kutoka kila upembe za kutaka achane na technologia ya kuunda Nukear,Iran imo mbioni kutengeneza mafuta ya Nuclear.
wakati huo huo waziri wa usalama wa Israel, Shaul Mofaz amesema kwamba nchi yake inaunga mkono juhudi za Umoja wa Ulaya za kibalozi juu ya mpango wa Iran wa nuklea .