Tehran. Shirin auangana na marekani kushutumu hatua za uchaguzi nchini Iran.
19 Juni 2005Matangazo
Mshindi wa nishani ya amani ya Nobel Shirin Ebadi , akirudia shutuma zilizotolewa na Marekani dhidi ya hatua za uchaguzi za Iran , amesema leo kuwa ataususia uchaguzi wa pili wa rais utakaofanyika siku ya Ijumaa.
Zaidi ya watu 1000 ambao wamejiandikisha kuwa wagombea katika uchaguzi nchini Iran hapo Juni 17 wamezuiwa kugombea na baraza la taifa la ulezi linaloangalia uchaguzi huo.
Wanawake wote waliotaka kugombea wameondolewa. Rais wa Marekani George Bush amesema kuwa uchaguzi huo sio wa haki kwa sababu ya kuzuiwa wagombea.