TEHRAN : Russia na Iran zasaini makubaliano ya nuklea
27 Februari 2005Matangazo
Russia imetia saini makubaliano ya kuipatia Iran mafuta ya nuklea kwa ajili ya mtambo wake wa kuzalisha umeme kwa nguvu za nuklea wa Bushehr.
Makubaliano hayo pia yanaitaka Iran kuirudishia Russia mafuta ya nuklea yaliokwishatumika.Waraka wa makubaliano hayo umetiwa saini katika mtambo wa Bushehr siku moja zaidi kufuatia siku iliyokuwa ikitegemewa kusainiwa.Maafisa wa serikali ya Marekani wanasema wanahofu kwamba mtambo huo wa Bushehr unaweza kutumiwa kama kisingizio na serikali ya Iran ili kutengeneza silaha za nuklea.
Iran inakanusha madai hayo kwa kusema kwamba mpango wake wa nuklia ni kwa ajili ya dhamira za amani tu.