TEHRAN: Mtetemeko wa ardhi nchini Iran
13 Machi 2005Matangazo
Mtetemeko wa ardhi uliokuwa na nguvu ya 5.9 katika mezani ya Richter umetokea Iran katika eneo la kusini-mashariki.Kwa mujibu wa IRNA-shirika rasmi la habari la Iran,mtetemeko huo umetokea aleo asubuhi katika jimbo la Sistan-Baluchistan mpakani na Pakistan.Gavana wa Saravan bwana Mohammad Mohebati amesema wasaidizi bado hawajafika katika vijiji vingi vilivyotawanyika katika jimbo hilo na kwa sababu ya uhaba wa mawasiliano ya simu,haijulikani hasa ni hasara gani ya maisha au mali iliyotokea.