TEHRAN: Miripuko ya bomu yasababisha hasara ya maisha nchini Iran
12 Juni 2005Matangazo
Mabomu 4 yalioripuka kusini-magharibi mwa Iran yameuwa si chini ya watu 5 na kuwajeruhi zaidi ya 80.Mabomu hayo yameripuka karibu na majengo ya serikali katika mji mkuu wa jimbo la Khuzestan,Ahvaz ambao mwezi wa April,ulishuhudia machafuko ya kikabila.Haijulikani ikiwa miripuko hiyo inahusika na machafuko ya April.Chama cha demokrasia cha Ahvaz,kinachopigania uhuru wa Khuzestan,kimekanusha kuhusika na miripuko hiyo.Hakuna aliejihusisha na mashambulio hayo yaliotokea siku tano tu kabla ya kufanywa uchaguzi wa rais nchini Iran.