TEHRAN: Mabomu yaripuka kusini-magharibi mwa Iran
12 Juni 2005Matangazo
Watu 3 wameuawa katika miripuko ya bomu iliyotokea kusini-magharibi mwa Iran.Mabomu hayo yameripuka katika mji wa Ahwaz ulio kiasi ya kilomita 500 kusini-magharibi mwa mji mkuu Tehran.Hakuna aliejitokeza na kutangaza kuhusika na miripuko hiyo,iliyotokea siku 5 tu kabla ya kufanywa uchaguzi wa rais nchini Iran.Mwezi wa April mji huo ulishuhudia machafuko ya kikabila,lakini haijulikani ikiwa miripuko hii ya bomu inahusika na machafuko hayo.