Tehran. Iran yatishia kuacha mazungumzo na mataifa ya Ulaya iwapo pendekezo lake halitakubaliwa.
20 Aprili 2005Matangazo
Iran imetishia kuacha mazungumzo na mataifa makuu ya Ulaya kutokana na mpango wake wa kinuklia kama mataifa hayo hayatakubali mapendekezo mapya ya serikali hiyo ya kuanza tena kurutubisha madini ya uranium hapo baadaye. Maelezo hayo yaliyotolewa na kiongozi wa baraza kuu la taifa la usalama, Hassan Rowhani ,yamekuja wakati waendesha majadiliano wanakutana mjini Geneva kujadili madai ya jumuiya ya Ulaya kuwa jamhuri hiyo ya Kiislamu iachane na mpango huo wa urutubishaji wa madini ya Uranium.
Mataifa matatu ya jumuiya ya Ulaya, Uingereza, Ujerumani na Ufaransa yamependekeza kwa Iran vivutio kama kama vya kiuchumi na kisiasa ili iweze kuachana na mpango huo. Iran inashikilia kuwa mpango wake wa kinuklia ni kwa matumizi ya kujipatia nishati.