Tehran. Iran yashutumiwa kwa matamshi ya rais wake.
28 Oktoba 2005Iran inakabiliwa na shutuma kali kutoka katika mataifa ya magharibi baada ya rais wake mwenye msimamo mkali Mahmoud Ahmednejad kusema kuwa Israel inapaswa kuondolewa kabisa katika ramani ya dunia.
Viongozi wa umoja wa Ulaya na Russia wamejiunga na Marekani na Canada katika kuyashutumu vikali matamshi ya Ahmedinejad.
Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ameonya kuwa serikali hiyo ya Iran inaweza kuadhibiwa.
Utawala wa Iran hadi sasa haujashutumu matamshi hayo, na kuamuru badala yake mabalozi wake watoe malalamiko yao rasmi dhidi ya mtazamo wa Ulaya kuhusu kile inachosema kuwa ni udhalimu wa Kiyahudi.
Kwa upande wake, Israel imeiita Iran kuwa ni kitisho wazi cha hivi sasa.