TEHRAN: Iran yaonya juu ya mpango wake wa Nuklear
16 Mei 2005Matangazo
Iran imesema huenda ikahairisha shughuli zake za kinuklea lakini ikasisitiza kwamba hatua hiyo ni ya muda tu ili kutoa nafasi ya duru mpya ya mazungumzo na Umoja wa Ulaya.
Hata hivyo Bunge la nchi hiyo limepiga kura kuipa wajibu serikali wa kutengeneza nishati ya Nuklea kwa ajili ya matumizi yake ya mitambo ya kuzalisha umeme hatua ambayo inapingwa na Marekani kwa madai kwamba Iran inataka kutengeneza silaha hatari.
Hapo mwezi wa Novemba mwaka jana Iran ilisimamisha mpango wake wa Nuklea kama ilivyokubaliana na mataifa Uingereza Ufaransa na Ujerumani.
Mataifa hayo matatu ya Ulaya yaliionya Iran kwamba ukiukaji wa makubaliano hayo huenda yakasababisha taathira mbaya kwa nchi hiyo.